Proverbs 3:1-6

Faida Nyingine Za Hekima


1 aMwanangu, usisahau mafundisho yangu,
bali zitunze amri zangu moyoni mwako,

2 bkwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako
na kukuletea mafanikio.


3 cUsiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe;
vifunge shingoni mwako,
viandike katika ubao wa moyo wako.

4 dNdipo utapata kibali na jina zuri
mbele za Mungu na mwanadamu.


5 eMtumaini Bwana kwa moyo wako wote
wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

6 fkatika njia zako zote mkiri yeye,
naye atayanyoosha mapito yako.

Copyright information for SwhKC